SHENG' NA USANIFISHAJI WAKE
Nilishangazwa ajabu Profesa Kimani Njogu, Profesa Mukoma wa Ngugi, Bi. Jane Obuchi na Kilolo Munyao waliposhabikia na kuwa makini kusikilizi mwandishi wa Sheng’ Felix Omondi akiwasilisha tafsiri yake ya kifungu cha bibilia tulichopewa kutafsiri wakati wa kongamano la Ituika agosti 12 mjini Naivasha. Pamoja na kwamba washiriki wengi walikuwa ama wandishi wa Kiswahili au wapenzi wake ukumbi ulichangamka wakati Felix Omondi alikuwa anatoa wasilisho lake. Binafsi sikutarajia kwani mara kwa mara jamii ya wapenzi wa Kiswahili imetaja sheng’ kuwa maradhi katika makuzi ya Kiswahili. Baada ya hapo tuliingia kwenye mjadala mkali ulioendelea hadi saa kumi asubuhi siku iliyofuatia. Majadiliano hayo yalihusisha Paul Nganga, Dr. Maina Mutonya, Dr. Kuria na Dr. Dosline. Miongoni mwa mengi yaliyojadiliwa ni wasilisho la Felix Omondi. Wanne hao walinifunza mimi jogoo wa shamba mengi nisiyoyajua kuhusu Sheng'. Kwanza ni kuwa Sheng' huwa na 'lahaja' zake kwa kutegemea sehemu au ene...