MATHIAS MOMANYI APENDEKEZA USAWA KATIKA TUZO ZA KISWAHILI
M.Momanyi :
“LINAYAVUNJA MATAIFA MENGINE MOYO… SAWAZISHA.
UTAIFA NI UPI?”
Mwanahabari Mathias Momanyi alitia doa kwenye uamuzi wa majaji wa Tuzo za Kiswahili
zinazothaminiwa na chuo kikuu cha Cornell, Shirika la Mabati Rolling na wakfu wa
Ngugi wa Thiong’o. Kwenye mkutano wa mtandaoni ulioshirikisha karibia watu mia
moja kutoka mataifa tofauti tofauti, wakenya walibaki vinywa wazi baada ya Profesa Abdilatiff Abdalla kufichua
kuwa washiriki wote waliotinga orodha ya saba bora walitoka katika taifa la
Tanzania. Isitoshe akiwapa moyo washiriki waliotuma miswada yao ila hawakufaulu
kuingia kwenye orodha hiyo, Prof. Alifichua kuwa asilimia 70 ya miswada yote
ilitoka katika taifa la Tanzania. Ufichuzi huo haukuwafurahisha baadhi ya
Wakenya waliokuwa mkutanoni, mwanahabari Mathias Momanyi akitoa hisia na mapendekezo yake kuhusiana na suala lenyewe.
“HAPA KAZI IPO... RIZIKI YAZIBWA AU YAWANIWA”
Momanyi alitaja mwelekeo huo kuwa wa kuvunja moyo wandishi
wa mataifa mengine kwa kukosekana kwa utaifa. Maoni yake yaliungwa mkono na
Harrison Bahati, Andati na wengineo. Momanyi alitilia shaka tamko la awali la profesa
kuwa washiriki walitoka katika mataifa mengine hasa majaji waliposema kuwa
hawakuwa na uwezo wa kuona majina wala nchi walizotoka washiriki.
“AWALI MLISEMA WASWIDI WAMEANDIKA, WAMAREKANI WAAZANIA NA
WENGINE SASA MMEBADILISHA NGOMA... HAMJUI WAANDISHI KATOKA WAPI?” Mathias
Momanyi
Hata hivyo mmoja wa majaji Salma Hamad alimjibu kwa kusema
kuwa wao (majaji) walipewa miswada bila
majina ila wandalizi kama Profesa Abdilatiff walikuwa na uwezo wa kuyatazama
majina na utaifa wa washiriki. Profesa alijaribu kutuliza joto kwa kusema kuwa
ikiwa mtu yeyote wa Afrika atautwaa ushindi basi bara zima limeshinda na hivyo
ipo haja ya kila mwafrika kufurahia.
Tukubali kuwa lugha hii hutumiwa katika nyanda mbalimbali za kawaida Tanzania.
ReplyDeleteHilo, hata hivyo halipaswi kuwa kigezo cha kuidhinisha unafiki na ubaguzi kwa msingi wa utaifa.
DeleteHivyo makosa ni ya nani? Waandalizi au majaji? Majaji walisema hawakuwa na uwezo wa kuona Majinaya washiriki...wao wanapewa miswada bila majina
DeleteTatizo kubwa ninaloliona katika waandishi Wakenya ni kwamba wanataka makuu, tuzo na kutambuliwa wakati wengi wao wanaandika kazi chapwa, hawana subira, hawakubali kushauriwa, wana viburi vya ajabu, dharau na ujeuri usio na kifani.
ReplyDeleteNaiona kesho iliyopangwa na Mungu. Ipo siku!
ReplyDeleteKuteleza ni kusonga mbele.
ReplyDeleteJinsia
ReplyDeleteJamani haifai kutuzwa kwa mjumbe ni wa utaifa. Washiriki wote wana nafasi ya kupewa nafasi sawa.
ReplyDeleteMsikateni tamaa tieni bidii na kesho hakika ushindi utakuwa wenu, cha muhimu kwa sasa ni umoja ambao ndio nguzo. Msitengane jamani.
ReplyDelete