MATHIAS MOMANYI APENDEKEZA USAWA KATIKA TUZO ZA KISWAHILI

 



M.Momanyi : 

“LINAYAVUNJA MATAIFA MENGINE MOYO… SAWAZISHA. UTAIFA NI UPI?”

Mwanahabari Mathias Momanyi alitia doa kwenye uamuzi wa majaji wa Tuzo za Kiswahili zinazothaminiwa na chuo kikuu cha Cornell, Shirika la Mabati Rolling na wakfu wa Ngugi wa Thiong’o. Kwenye mkutano wa mtandaoni ulioshirikisha karibia watu mia moja kutoka mataifa tofauti tofauti, wakenya walibaki vinywa wazi  baada ya Profesa Abdilatiff Abdalla kufichua kuwa washiriki wote waliotinga orodha ya saba bora walitoka katika taifa la Tanzania. Isitoshe akiwapa moyo washiriki waliotuma miswada yao ila hawakufaulu kuingia kwenye orodha hiyo, Prof. Alifichua kuwa asilimia 70 ya miswada yote ilitoka katika taifa la Tanzania. Ufichuzi huo haukuwafurahisha baadhi ya Wakenya waliokuwa mkutanoni, mwanahabari Mathias Momanyi akitoa hisia na mapendekezo yake kuhusiana na suala lenyewe.  

“HAPA KAZI IPO... RIZIKI YAZIBWA AU YAWANIWA

Momanyi alitaja mwelekeo huo kuwa wa kuvunja moyo wandishi wa mataifa mengine kwa kukosekana kwa utaifa. Maoni yake yaliungwa mkono na Harrison Bahati, Andati na wengineo. Momanyi alitilia shaka tamko la awali la profesa kuwa washiriki walitoka katika mataifa mengine hasa majaji waliposema kuwa hawakuwa na uwezo wa kuona majina wala nchi walizotoka washiriki.

“AWALI MLISEMA WASWIDI WAMEANDIKA, WAMAREKANI WAAZANIA NA WENGINE SASA MMEBADILISHA NGOMA... HAMJUI WAANDISHI KATOKA WAPI?” Mathias Momanyi

Hata hivyo mmoja wa majaji Salma Hamad alimjibu kwa kusema kuwa wao (majaji)  walipewa miswada bila majina ila wandalizi kama Profesa Abdilatiff walikuwa na uwezo wa kuyatazama majina na utaifa wa washiriki. Profesa alijaribu kutuliza joto kwa kusema kuwa ikiwa mtu yeyote wa Afrika atautwaa ushindi basi bara zima limeshinda na hivyo ipo haja ya kila mwafrika kufurahia.

 


Comments

  1. Tukubali kuwa lugha hii hutumiwa katika nyanda mbalimbali za kawaida Tanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hilo, hata hivyo halipaswi kuwa kigezo cha kuidhinisha unafiki na ubaguzi kwa msingi wa utaifa.

      Delete
    2. Hivyo makosa ni ya nani? Waandalizi au majaji? Majaji walisema hawakuwa na uwezo wa kuona Majinaya washiriki...wao wanapewa miswada bila majina

      Delete
  2. Tatizo kubwa ninaloliona katika waandishi Wakenya ni kwamba wanataka makuu, tuzo na kutambuliwa wakati wengi wao wanaandika kazi chapwa, hawana subira, hawakubali kushauriwa, wana viburi vya ajabu, dharau na ujeuri usio na kifani.

    ReplyDelete
  3. Naiona kesho iliyopangwa na Mungu. Ipo siku!

    ReplyDelete
  4. Jamani haifai kutuzwa kwa mjumbe ni wa utaifa. Washiriki wote wana nafasi ya kupewa nafasi sawa.


    ReplyDelete
  5. Msikateni tamaa tieni bidii na kesho hakika ushindi utakuwa wenu, cha muhimu kwa sasa ni umoja ambao ndio nguzo. Msitengane jamani.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SHENG' NA USANIFISHAJI WAKE